Jeremiah 51:44-49


44 aNitamwadhibu Beli katika Babeli,
na kumfanya atapike kile alichokimeza.
Mataifa hayatamiminika tena kwake.
Nao ukuta wa Babeli utaanguka.


45 b“Tokeni ndani yake, enyi watu wangu!
Okoeni maisha yenu!
Ikimbieni hasira kali ya Bwana.

46 cMsikate tamaa wala msiogope tetesi
zitakaposikika katika nchi;
tetesi moja inasikika mwaka huu,
nyingine mwaka unaofuata;
tetesi juu ya jeuri katika nchi,
na ya mtawala dhidi ya mtawala.

47 dKwa kuwa hakika wakati utawadia
nitakapoziadhibu sanamu za Babeli;
nchi yake yote itatiwa aibu,
na watu wake wote waliouawa
wataangukia ndani yake.

48 eNdipo mbingu na dunia na vyote vilivyomo ndani yake
vitapiga kelele za shangwe juu ya Babeli,
kwa kuwa kutoka kaskazini
waharabu watamshambulia,”
asema Bwana.


49 f“Babeli ni lazima aanguke kwa sababu ya kuwaua Waisraeli,
kama vile waliouawa duniani kote
walivyoanguka kwa sababu ya Babeli.
Copyright information for SwhKC